Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewaonya Mawakala wote wanaojihusisha na usambazaji wa mbolea ya ruzuku Mkoani Njombe kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa wakulima kuhujumu zoezi la ununuzi wa mbolea ya ruzuku kuacha mara moja tabia hiyo na kuheshimu biashara zao.
Mtaka amesema hayo katika kikao maalumu kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya Wananchi juu ya uwepo wa hujuma katika zoezi zima la usambazaji mbolea ya ruzuku huku Serikali ikiwa imetoa kiasi cha shilingi bilioni 150 kupunguza makali ya mbolea kwa wakulima ili kila mkulima aweze kunufaika kupitia ruzuku hiyo.
“Upo mchezo ambao Mawakala mnaufanya wa kusajili wakulima hewa na kuwapatia fedha kiasi cha shilingi elfu kumi kumi. Hatutalipa hela Wakala hewa. Na kama yupo wakala humu anayewapatia wakulima fedha kiasi cha shilingi elfu kumi wajisajili majina ya uongo umeamua kuiingiza biashara yako shimoni. Umeamua kufanya biashara ya mbolea fanya kwa nidhamu na heshimu biashara yako. Hatutakubali nia njema ya Serikali, nia njema ya Mheshimiwa Rais ya kutoa mbolea ya ruzuku kwa lengo la kuwasaidia wakulima halafu mtu aje afanye mchezo kwenye mbolea hii.”Alisema Mtaka
Aliendelea kusema “Kama umejiandaa kufilisika fanya mchezo na mbolea ya ruzuku. Hautajijirikia mbolea ya ruzuku ya mwaka huu.Hii ni mbolea iliyotolewa na Serikali kwa lengo la kuwasaidi Wananchi wake. Kama kuna Wakala hapa aache mara moja. Kwenye hili hakuna rangi tutaacha kuona Mheshimiwa Rais amezungumzia suala la Mbolea ya ruzuku kwa mara ya kwanza akiwa Mbeya na kwa mara ya pili amezungumzia katika Mkoa wa Njombe na Mheshimiwa Waziri sipo tayari kuona hujuma katika mbolea hiyo.”Alisema.
Wakizungumza katika nyakati tofauti tofauti baadhi ya wasambazaji wa mbolea wamesema kuwa zipo changamoto kadha wa kadha zinazowakabili kwenye usambazaji wa mbolea hizo ikiwa ni pamoja na makampuni yanayoingiza mbolea Nchini kushindwa kuchagua mawakala licha ya Mawakala hao kutuma maombi na pia upatikanaji wa mbolea hizo umekuwa si wa kuridhisha na wengine kushindwa kutoa baadhi ya mbolea kwa Mawakala hao.
Aidha Wadau hao wameomba Wakala wa Usimamizi wa Mbolea Nchini NFRA kuhakikisha kuwa katika viwango vya ujazo wa mbolea za ruzuku kuwa na ujazo mdogo ili kila Mkulima aweze kunufaika na pia kuongeza kasi ya usajili wa Wakulima hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye msimu wa Kilimo ambapo mahitaji ya mbolea ni mengi.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mbolea NFRA amesema kuwa kwa sasa NFRA imeboresha mfumo wa usajili wa wakulima kwenye zoezi hilo ambapo kwa sasa zoezi hilo linafanywa na Maafisa Ugani ngazi ya Wilaya huku malengo kwa siku ikiwa ni usajili wa wakulima 2000 kwenye mfumo.
Aidha kuhusu upatikananji wa mbolea za ruzuku kwa ujazo wa mdogo wa kilo 5 na kumi Mwakilishi huyo amesema kuwa jambo hilo nalo litaanza kupatikana kwenye mfumo siku za karibuni kutokana na kuwa wakulima wengi wamekuwa na maombi ya kupatiwa mbolea zenye ujazo huo.
Awali akiwasilisha taarifa ya usambazaji wa mbolea na uandiksihaji wa wakulima katika Mkoa wa Njombe Afisa Kilimo Mkoa wa Njombe Joel amesema kuwa Mkoa umeweka malengo ya kuwasajili wakulima 214, 870 kwa Mkoa mzima ambapo wakulima walioandikishwa na kutambuliwa kwenye daftari ni wakulima 160,752 na waliosajiliwa kwenye mfumo tayari kwenda kuchukua mbolea ya ruzuku ni Wakulima 99,645 sawa na asilimia 46.5 na Wakulima waliokwisha pata mbolea ni Wakulima 11,682 sawa na asilimia 5 ya Wakulima waliokwisha pata mbolea.Huku kiasi cha mbolea kilichokwisha pokelewa kikiwa ni tani 3556.8.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe