Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abasi amepongeza hatua ya Mkoa wa Njombe kutoa elimu kwa njia ya mabango kuhusu athari na uthibiti wa moto kichaa janga ambalo linapoteza mabilioni ya uchumi wa Wananchi Mikoa ya kusini ikiwa miongoni mwa waathirika wakubwa.
Kanali Ahmed amesema hayo wakati alipotembelea banda la Mkoa wa Njombe na kuangalia shughuli za utalii zinazofanyika Mkoani humo wakati wa maonesho ya utalii kusini; Mkoa wa Njombe ukiwa miongoni mwa washiriki.
“Niwapongeze sana kwa hatua hii ya kutembea na mabango kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuacha uchomaji wa misitu.Tumekuwa waathirika wakubwa wa matukio ya moto yanayotokea katika Mikoa yetu na kupoteza uchumi wa mikoa hiyo kutokana na janga la moto. Niwapongeze kwa ubunifu huu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii” Alisema Kanali Ahmed
Aidha Kanali Ahmed amesema kuwa elimu ya majanga ya moto ni muhimu kuendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali ili jamii iweze kuwa na uelewa juu ya athari zitokanazo na janga hilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe