Aprili 2,2024 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka ameongoza kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Kamati ilitoa maagizo 12 wakati wa kujadili hesabu za fedha za halmashauri za mwaka 2021/2022 kwa halmashauri nne za mkoa wa Njombe ambazo ni,Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Halmashauri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe aidha maagizo 5 yalikuwa ya miaka ya nyuma.
Mkoa wa Njombe kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ulikuwa na jumla ya hoja 162 hoja za kitabu kikubwa zilikuwa 115 kitabu cha afya 26 na mfuko wa wanawake 26 kati ya hizo hoja 117 zimejibiwa na kufungwa na kubakia na hoja 45, 35 zikiwa ni za kitabu kikubwa 3 za mfuko wa afya na 7 za mfuko wa wanawake, vijana na ulemavu.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya,makatibu Tawala wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri sita (6) za mkoa pamoja na wajumbe wanaounda kamati ya fedha kwenye kila Halmashauri pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe