• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Halmashauri ya Mji Njombe
Halmashauri ya Mji Njombe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Halmashauri ya Mji Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

RC Njombe azitaka Halmasahuri kuwa na vyanzo vya kibunifu kwenye mapato

Tarehe iliyowekwa: November 2nd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amezitaka Halmashauri kuwa na mawazo ya kipekee na kibunifu juu ya kuanzisha  vyanzo vipya  vya mapato vya Halmashauri badala ya kuwa na mawazo ya kutegemea vyanzo ambavyo vinaweza kufikia ukomo wakati wowote.

Akizungumza katika kikao  kazi maalumu kilichojumuisha Viongozi na Watendaji kutoka Wilaya ya Njombe  Mtaka amesema kuwa Halmashauri zimeshindwa kuwekeza kwenye mawazo  ya kibunifu na kuwa na vyanzo vya kiuwekezaji na hivyo kushindwa kuongeza mapato maradufu ya mapato yanayokusanywa sasa.

"Zipo Halmashauri ambazo zimeanzisha miradi ya kiuwekezaji kama hoteli, kumbi za sherehe, mikutano, uwekezaji kwenye Ardhi,Viwanda.Ni vyema kujifunza kwa wenzetu na kuona wao wamefanya nini ili na sisi tuweze kuwa na ukusanyaji wenye tija badala ya kutegemea makusanyo ambayo muda wowote chanzo unachokusanya kinaweza kisiwepo na hivyo kukusababishia kukosa mapato"Alisema Mtaka

Mtaka aliendelea kusema kuwa suala la kuongeza  ukusanyaji mapato limekua ni jambo la kawaida lakini kwa sasa timu za kitaalamu za halmashauri na kamati za fedha na mabaraza ya Madiwani inabidi kubadilika na kuja na mitazamo mipya ya kuongeza marambili thamani ya  makusanyo yaliyokuwa yanakusanywa kwenye Halmashauri awali.

Akichangia hoja katika kikao Kazi hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Erasto Mpete amesema kuwa Halmashauri ya Mji Njombe inamipango ya kufanya uwekezaji wenye tija na tayari ipo katika mipango ya kuwa na maeneo ya maegesho ya malori, kumbi za sherehe, Ujenzi wa Shule za kisasa za mchepuo wa kiingereza ili kuweza kuwa na vyanzo vya kudumu kwenye ukusanyaji mapato.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa  Halmashauri ya Mji Njombe kimehusisha Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa,Maafisa Tarafa,Watendaji wa Vijiji na Mitaa na Viongozi mbalimbali wote kutoka Wilaya ya Njombe
















Matangazo

  • KUITWA KAZINI NA MAFUNZO TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 21, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 19, 2025
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTAKA AONGOZA MAOMBI YA AMANI KWA TAIFA.

    November 07, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO NJOMBE MJINI AFUNGUA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA .

    October 26, 2025
  • MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA 366 WAAPISHWA NA KUPATIWA MAFUNZO JIMBO LA NJOMBE MJINI.

    October 25, 2025
  • KUBWA KULIKO KUWAHI KUTOKEA NJOMBE MJINI

    October 20, 2025
  • Angalia zote

Video

TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe