Kamati ya ulinzi wa Mwanamke na Watoto katika Halmashauri ya Mji Njombe imepatiwa mafunzo yaliyolenga kuboresha utoaji huduma ya kisaikolojia kwa jamii ili kuweza kukabiliana na majanga kikamilifu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkazi kutoka shirika la REPSSI Edwick Mapalala amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani makundi ya Wanawake na Watoto yamekuwa yakikabiliana na ukatili mkubwa ndani ya jamii huku kundi hilo likiwa ndio waathirika wakubwa zaidi.
Wakiwasilisha mada mbalimbali juu ya utoaji wa huduma ya kisaikolojia kwa makundi maalumu wawezeshaji wa mafunzo hayo wamesema kuwa katika vipindi vya majanga mfano milipuko ya magonjwa,vita,mafuriko wanawake,watoto,wazee na watu wenye ulemavu wamekuwa wakiathiriwa na majanga yanayotokea na hivyo kamati ya ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto inatakiwa kuhakikisha kuwa inakuwa na uelewa wa kutosha juu ya utoaji wa huduma ya kisaikolojia ili kuweza kujiandaa wakati majanga yanapotokea.
Miongoni mwa mambo yaliyozua mjadala katika mafunzo hayo ni pamoja na sheria ya mtoto chini ya miaka 18 anapomfanyia ukatili wa kingono mtoto mwenzake ambapo mwalifu huweza kupewa adhabu ya viboko au kulipa faini jambo linaloonekana kama ni uonevu kwa mtoto aliyefanyiwa ukatili na wameiomba Serikali kuona ni kwa namna gani sheria ya mtoto chini ya miaka 18 inaweza kufanyiwa maboresho kwani kwa sasa mtoto wa chini ya miaka 18 anaweza anakuwa tayari amepevuka na anauwezo wa kumpa mimba mtoto mwenzie hivyo ni vyema umri ukapunguzwa na adhabu pia ikaongezwa tofauti na hali ilivyo sasa.
Mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, kamati iliweza kuandaa mpangokazi wa Halmashauri wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo miongoni mwa majukumu ya kusimamia dhana muhimu zinazohusiana na ulinzi na usimamizi wa kamati ngazi ya Kata pia kamati itawatambua wadau mbalimbali ili kuweza kushirikiana katika kuleta nguvu ya pamoja na kutekeleza mipango ya ulinzi na utoaji wa msaada wa kisaikolojia na elimu kwa jamii na hatimaye jamii iweze kuelimika na kutokomeza masuala ya ukatili kikamilifu
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe