Wanawake wametakiwa kutofumbia macho vitendo rushwa haswa rushwa ya ngono inayozalilisha utu wa mwanamke.
Rai hiyo imetolewa Machi 08,2024 na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Scholastica Assey katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika kimkoa katika kijiji cha Usita Wilayani Wanging’ombe.
Amewataka wanawake kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa zinazohusu vitendo vya rushwa kwa kuwa suala la rushwa ni suala linalowagusa kila mmoja.
"Masuala ya rushwa yanatugusa wanawake haswa rushwa ya ngono,tusikae kimya inapotokea umeombwa rushwa haswa kwenye maeneo ya kazi toa taarifa haraka kupitia namba ya bure 113, suala hili linatudhalilisha kama wanawake". Alisema Bi. Scholastica.
Aidha amehimiza wanawake kuwa vinara wa ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha hakuna ubadhirifu unaotokea ili miradi hiyo iwe na tija kwa jamii.
Akiendelea kuzungumza Bi. Scholastica amesema ni muhimu kwa wanawake wote kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2024 na uchaguzi mkuu ujao na kuzingatia kutojihusisha na vitendo vya rushwa kipindi chote cha uchaguzi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe