Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka Disemba 21,2023 wakati wa mkutano na Msemaji Mkuu wa Serikali pamoja na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita Mkoani Njombe amesema, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imewasikia wananchi wa Njombe na kuwafikia katika kutatua kero zao kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Maji,Barabara ,kilimo,elimu na Afya.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara na maji,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwakuwa Mkoa wa Njombe ni moja ya Mikoa inayonufaika na mradi mkubwa wa maji ambao utatatua changamoto ya maji kwa wananchi kwa asilimia 95,pamoja na miradi ya barabara ambapo ameishukuru Serikali kwa kuboresha mtandao wa barabara na kufanya maeneo mengi ya Mkoa wa Njombe kufikika kwa kuwa na barabara zenye kiwango cha lami.
Aidha ameipongeza Serikali na maono ya Rais kwa kuona umuhimu wa kulipa fidia ya bilion 15 kwenye maeneo yenye makaa ya mawe na madini ya chuma Wilayani Ludewa sambamba na ujenzi wa barabara kubwa ya zege ambayo itafungua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe.
Pia ameipongeza Serikali kwa kutoa mbolea za ruzuku kwa wakulima jambo ambalo litasaidia kuendelea kuinua uchumi wa wananchi Njombe na kusaidia kuchangia kwenye pato la Mkoa na Taifa.
Katika sekta ya elimu Mheshimiwa Mtaka ameeleza namna Serikali ilivyofanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu jambo ambalo ni ishara ya mageuzi makubwa kwenye elimu Mkoani Njombe kwakuwa kila kata Mkoani Njombe ina shule ,hivyo kuwezesha watoto wote wanaofaulu kuweza kuendelea na masomo.
Kwenye sekta ya afya Mkuu wa Mkoa Mtaka ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa namna ambavyo imesogeza huduma karibu na wananchi na kuhakikisha Hospitali zote zinafanya kazi zikiwa na vifaa ,madawa ,watumishi na vitendea kazi vingine vinavyowezesha huduma kupatikana wakati wote.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe