Halmashauri ya Mji Njombe imetoa dawa za viuatilifu kwa wakulima wa kata ya Uwemba,Luponde ,Matola Lugenge na Utalingolo kwa ajili ya kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao (viwavijeshi) ambavyo vimeshambulia mazao shamabani.
Akizungumza Januari 30,2024 Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Njombe Peter Magehema mara baada ya kukabidhi dawa hizo kwa wakulima ameweka bayana nama Serikali ilivyopambana kutokomeza wadudu hao ambao wanaharibu mazao ya wakulima.
Kwa Halmashauri ya Mji Njombe Serikali imetoa viuatilifu hivyo kwa hekta 4000 ambazo zitapelekwa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoathiwa na wadudu hao.
Akiendelea kuzungumza Bwana Magehema amesema kutokana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na wadudu hatari sana ambao wanashambulia mazao ya kilimo ambapo kwa sasa Serikali imetoa dawa za ruzuku bure kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ili kuweza kunusuru mazao yao.
Kwa upande wake Wino Mlowe Mwenyekiti wa Kijiji cha Itulila Kata ya Matola kwa niaba ya wananchi wa maeneo ya Kijiji hicho ameishukuru Serikali kwa namna inavowajali wakulima ambao wanakabiliana na changamoto za wadudu hao pamoja na kupewa dawa za viuatilifu bure kwa wakulima waeneo hayo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe