Halmashauri ya Mji Njombe imetoa zawadi ya shilingi laki tano na cheti kwa shule ambazo zimefanya vizuri kwenye mtihani ya taifa kwa mwaka 2023
Akizungumza Machi 22,2024 mara baada ya ugawaji wa zawadi hizo Mhe.Kissa Gwakisa Kasongwa amewapongeza waalimu wote wa shule ambazo zimefanya vizuri akizitaka shule ambazo hazikufanya vizuri kuendelea kufundisha kwa bidii ili kufikia malengo ambayo yamewekwa.
Shule za msingi zilizopata zawadi ni MT Bakita ,Senga,Mdete ,Gilgali , St Getrude na shule za sekondari ni Kilocha Seminari ,Romani Boys, Josephine Girls ,Anne Makinda, Mbeyela , Yakobi ,na Mgola
Akiasilisha taarifa ya hali ufaulu kwa shule za Halmashauri ya Mji Njombe, Huruma Chaula Afisa Elimu Sekondari alieleza kuwa kwa mwaka 2023 katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) ufaulu ulikuwa asilimia 92.6%, kidato cha nne ufaulu ulikuwa asilimia 94% na kidato cha sita ufaulu ulikuwa asilimia 99.9%.
Halmashauri ya mji Njombe kwa mwaka 2024 imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha ufaulu unaongezeka hadi kufika 95% kwa watahiniwa wa darasa la saba na kufuta daraja sifuri na F kwa sekondari na ufaulu wa kuanzia Daraja la I-III kuwa na zaidi ya 50%.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe