Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick anawatangazia wananchi wote wa Kata ya Kifanya kuwa kuanzia tarehe 8 hadi 21 Oktoba, kutafanyika Kliniki ya Ardhi katika ofisi ya kijiji cha Kifanya.
Katika kipindi hicho, wananchi watapatiwa huduma mbalimbali za ardhi pamoja na kupokea, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi na masuala mengine ya huduma zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.
Aidha, kutakuwepo na dawati la malalamiko na msaada wa kisheria kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika katika usuluhishi kupata haki zao.
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu ili kuepukana na migogoro ya ardhi isiyo ya lazima kwa maendeleo endelevu.
Uonapo tangazo hili, tafadhali mjulishe na mwingine.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe