Dkt. Biteko amesema hayo Mei 26,2024 kwenye uzinduzi wa kampeni ya huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaing) itakayofanya kazi kwa siku 10 katika Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe.
Aliwataka wananchi kuacha misimamo iliyopitiliza wakati timu ya mawakili itakapokuwa inawasikiliza na badala yake wafuate ukweli.
“Maandiko yanasema ukijua kweli itakuweka huru nawe utakuwa huru kweli kweli, mawakili simamieni ukweli mtapokuwa mnasikiliza watu hawa watakaokuja kwenu,”Alisema Dkt.Biteko.
Mhe.Biteko alibainisha nia ya Serikali kwenye kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi haswa wale wasioweza kumudu gharama za kisheria katika utatuzi wa migogogro kwa njia mbadala nakutoa rai kwa wananchi kutumia vizuri fursa hiyo.
“ Niwaombe wananchi wa Tanzania kupitia kampeni hii,wale ambao hawawezi kumudu gharama za mawakili wachukue fursa hii kuwaona wataalamu wetu wa kisheria, waweze kusikilizwa nakupatiwa ushauri na hatimaye kumaliza migogoro hii”.Alisisitiza Dkt Biteko .
Katika hatua nyingine alitoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa na kutafuta msaada wa kisheria mapema ili migogoro inayoibuka kwenye jamii itatuliwe kabla yakuwa na madhara.
“Ili tuwe na jamii ambayo ina stahimiliana,jamii ambayo watu wake hawana migogoro mingi, ni muhimu migogogro ikatatulia mapema ,tukisubiri watu wameapizana wamefika mbali ,hata hawa wataalamu wanaokuja huko watakuja kushughulika na kisasi badala yakutafuta suluhu”.Alisema.
Akihitimisha hotuba yake alitoa wito viongozi kwa viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaofanya kazi ngazi ya kata na vijiji ili kufanya kazi iwe rahisi na kutimiza lengo la kampeni hiyo.
Kauli mbiu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaing) inasema Msaada wa Kisheria kwa Haki,Usawa,Amani na Maendeleo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe