Wananchi Mkoani Njombe watakiwa kujikita katika malezi kwa watoto ili kuweza kuondokana na udumavu ambao umekuwa changamoto .
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikisa Kata ya Uwemba Halmashauri ya Mji Njombe katika Mkutano wa Hadhara Mhe Deo Mwanyika Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanawalisha watoto wao milo kamili ili kuweza kuepukana na Udumavu.
"Ni aibu kuona kwenye familia kuna mtoto anaudumavu , Niombe wazazi na walezi kila mmoja wetu akawe kipaumbele katika malezi ya familia yake kwasababu tukiwa na watoto wadumavu basi tutakuwa na kizazi chenye udumavu" Mhe Deo Mwanyika Mbunge Jimbo la Njombe Mjini.
Aidha katika mkutano huo Mhe Mwanyika ametoa miche ya parachichi 800 kwa baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ikisa na Uwemba kwa ajili ya kupunguza changamoto ya udumavu kutokana na wanachi kutokula matunda kwa wingi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amewaomba wananchi wa Kijiji cha Ikisa kuendelea kimuunga mkono Mhe. mbunge katika utendaji wa kazi kutokana na juhudi mbalimbali za kuwaletea maendeleo zinazofanyika.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe