Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema hayo Leo agosti 10, wakati wa uzinduzi wa soko kuu Njombe lililogharimu kiasi Cha Shilingi Bilioni 10.2
"Adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inarasimisha sekta isiyo rasmi.Wanaofanya katika soko kuu Njombe hawàkuwa rasmi lakini mara baada ya Ujenzi wa soko hili, wamewekwa sehemu Moja, wanafanya Kazi katika eneo Moja huduma zote zipo kwa hiyo hawa ni rami sasa"Alisema Rais
Akizungumzaia ujenzi wa soko hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema ujenzi wa soko hilo umegharimu Sh10.2 bilioni.
Waziri Bashungwa amesema “Soko hili litawasaidia wafanyabiashara kufanya bishara zao mahali pazuri, hasa wajasiriamali.
“Mjasiriamali mdogo atalipa Sh10, 000 kwa kila mwezi kwa upande wa vizimba na hiyo ndio dhamira na maelekezo ya Rais Samia anapozungumzia kuweka maziringa rafiki kwa wafanyabiashara ndogondogo” amesema Bashungwa.
Soko hilo la kisasa lina ukubwa wa mita za mraba 9,186 lina sakafu (floors) tatu na Soko lina mifumo na sehemu mbalimbali yakiwemo maduka 162, meza za biashara 407, vyoo 47, migahawa 2, stoo 6, vizimba vya kuku 27, machinjio ya wanyama wadogo, sehemu za huduma za kibenki 2, ofisi za utawala 2, mfumo wa maji safi na maji taka, kisima kirefu cha maji.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe