Wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Njombe zilizofanyika Juni 17,2024 ,wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipatiwa huduma za afya ikiwemo upimaji na ushauri katika viwanja vya stendi ya zamani vilivyopo Njombe Mjini.
Jumla ya watu waliopimwa virusi vya Ukimwi ni 103 ,wanawake wakiwa ni 34 na wanaume 69 kati yao wanaume 2 na mwanamke 1 sawa na asilimia 2 waligundulika kuwa na Virusi vya Ukimwi nakushauriwa kisha kukubaliana kuanza matumizi ya dawa.
Kwa upande wa uchangiaji wa damu salama ,jumla ya watu 41 wanaume wakiwa 33 na wanawake 8 walijitokeza kuchangia damu uniti 41.
Katika upimaji wa hali ya Lishe watu 32 walipimwa hai zao za lishe na kati ya hao 24 walikuwa na hali nzuri ya Lishe ,7 walikuwa na uzito uliozidi na 1 alikuwa na uzito uliozidi sana.Watu wote waliweza kushauriwa ili kuendelea kuboresha hali zao za lishe.
Na kwa upande wa Malaria jumla ya watu 72 walipewa elimu ya kujikinga na malaria pia watoto 10 wenye umri chini ya miaka 5 walipatiwa vyandarua.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zinaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe