Agosti 5, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amezitaka taasisi za serikali zinazoshiriki maonesho ya Nanenane kuhakikisha zinakuwa na ubunifu wa teknolojia ya kisasa, ili kuendana na mabadiliko ya sayansi.
Akizungumza alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho hayo katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, Mhe. Mtaka alisema kuna haja ya taasisi sa serikaki kuachana na mazoea ya kuonesha vitu vya kizamani ambavyo havina tija kwa mkulima wa sasa.
"Taasisi za serikali zinapaswa kutoka kwenye mtazamo wa zamani na kuja kwa kisasa, tunahitaji kuona zikiwasilisha suluhisho la ubunifu na teknolojia zinazoendana na wakati huu nasio kurudia kila mwaka yale yale," alisema Mhe. Mtaka Mkuu wa Mkoa Njombe.
Aidha Mhe. Mtaka meongeza kuwa ni muhimu kwa taasisi hizo kuzingatia sera zinazolingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ili kuhakikisha mchango wao unaendana na mwelekeo wa kitaifa wa kukuza uchumi wa kilimo, viwanda na teknolojia huku akizitaka taasisi zinazowasilisha zana na teknolojia za kilimo katika maonesho ya Nanenane kuhakikisha zinafanya tathmini sahihi ya maeneo husika kabla ya kupeleka teknolojia hizo.
"Hatuwezi kupeleka teknolojia ya umwagiliaji wa matone sehemu yenye mvua nyingi au kupeleka trekta kubwa eneo la kilimo cha bustani ya familia. Tunahitaji uhalisia," alisisitiza Mhe. Mtaka
Maonesho ya Nanenane mwaka huu 2025 yameenda kwa kaulimbiu “chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025.”
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe