Waziri wa utamaduni, sanaa na michezo Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana katika siku ya pili ya Tamasha la Pili la Utamaduni Kitaifa Agosti 26, 2023 amekagua mabanda ya maonesho ya Utamaduni na Sanaa pamoja na huduma mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali, Fedha na Wadau wengine
Mhe. Waziri Dkt. Pindi Chana katika siku hii ya pili aliongozana na viongozi mbalimbali kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko, viongozi wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Wakuu wa Idara za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Vikundi mbalimbali vilivyoshiriki tamasha la pili la utamaduni vipo kwenye mashindano ambayo yanahitimishwa na mshindi kutajwa Agosti 26,2023.
Miongoni mwa vikundi vilivyofanikiwa kuingia hatua ya sita bora ni vikundi kutoka mkoa wa Ruvuma ,Dodoma ,Zanzibar ,Njombe ,Mwanza na Mtwara.
Kauli mbiu ya tamasha la utamaduni inasema “Utamaduni ni msingi wa madili tuulinde na kuuendeleza”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe