Julai 22, 2025 Robert Sabwoya, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ameongoza timu ya wataalamu kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Njombe kwa ajili ya kukagua na kutathmini utekelezaji wa miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1,290,180,028.
Akiwa katika ziara hiyo Bw. Sabwoya amesema ziara hiyo imelenga kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa wakati na viwango vya ubora vinavyotakiwa, na kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zinazotilewa
Alieleza kuridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa miradi hiyo, huku akiupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia thamani ya fedha.
“Tunaipongeza halmashauri kwa juhudi hizi. Tumeona kasi nzuri ya maendeleo na matumizi mazuri ya rasilimali,” alisema Bw. Sabwoya.
Aidha, amehimiza uongozi wa halmashauri kuendeleza juhudi hizo za kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.
Timu hiyo ya wataalamu iliweza kutembelea nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe,Nyumba ya Mwalimu shule ya sekondari Makowo, Shule Mpya ya Sekondari Wikichi na Shule ya mpya ya Mapinduzi iliyopo kata ya Iwungilo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe