Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) Wilaya ya Njombe umetakiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemeo kukatika kwa mawasiliano kwenye baadhi ya barabara zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe ili kuwezesha barabara hizo kupitika wakati wote na kuondoa kero kwa wananchi haswa msimu huu wa mvua.
Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mheshimiwa Filoteus Mlingo wakati akifunga mkutano wa baraza la madiwani kujadili taarifa za kata Januari 30,2024.
Mhe.Mligo ameutaka wakala huo kuhakikisha unafanya mawasiliano na uongozi wa kata ili kurahisisha utendaji na kuwataka wakandarasi wanaokabidhiwa maeneo kuhakikisha wanaripoti na kuwa na barua ya utambulisho kwa viongozi wa kata akiwemo diwani husika kabla yakuanza kazi.
“Watu wa TARURA barabara zetu huko ni chafu kweli kweli, ni mbaya hembu twende tukapitie ,kwa mfano barabara ya Zengerendete ,Utalingolo, kisilo kwenda Luponde mkandarasi ameanza kulima ameharibu baadhi ya eneo limekatika, sasa maeneo yale ni kwenda kuona tuone namna gani yakurekebisha haraka”Alisema Mhe. Mligo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Luponde Mhe.Ulrick Msemwa na diwani wa kata ya Uwemba Mhe.Jactan Mtewele wameshauri kutokana na ufinyu wa bajeti ni vyema TARURA kuhakikisha barabara zinatengezwa kwa ubora unaotakiwa ili zidumu kwa muda mrefu aidha wapate fursa yakukaa na wenyeji ili kuweza kufahamu wakati sahihi na maeno ambayo yanahitaji matengenezo ya haraka ili kuondoa kero kwa wananchi haswa kipindi cha msimu wa mvua.
Aidha suala la kampeni yakuhamasisha lishe bora kwenye jamii ili kupambana na udumavu ndani ya Halmashauri ya Mji NJombe limesisitizwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Filoteus Mligo, akiwataka waheshimiwa madiwani kuweka agenda ya lishe kwenye mikutano yao ya kata.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe