Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wakunusuru kaya masikini Halmashauri ya Mji Njombe, umeanza kutekeleza mradi wa kuongeza kipato IGA (Income generation activities) kwa walengwa ambao watapatiwa kuku wa kienyeji 10 kwa kila kaya ili kujikwamua na umasikini.
Akizungumza Mei 11,2024 wakati wa ugawaji wa kuku 50 kwa kaya 5 wanufaika wa TASAF wa Vjiji na Mitaa ya Wikichi ,Magoda na Itulike, Mariamu Monjesa Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji Njombe amesema,
" Lengo la kugawa kuku kwa wanufaika hawa nikuwasaidia kupata mitaji kutokana na hali duni ya ugumu wa maisha pamoja na kuwatengenezea kipato cha kudumu kitakachowawezesha kuanzisha miradi mingine ya maendeleo baada ya kuku hawa kuzaliana".
Aidha Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji Njombe amewaombwa wanufaika hao kwenda kutekeleza miradi hiyo kama ilivyo pangwa na sio kwenda kutumia tofauti na malengo ya mradi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe