Wanafunzi wa kike 8,552 wa Shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 15,000,000/= zitakazoenda kuboresha maendeleo ya taaluma zao.
Akizungumza Februari 28 ,2024 katika hafla hiyo ya ugawaji wa taulo hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete amewataka walimu wote ambao walifika kupokea taulo hizo kwenda kupeleka kwa walengwa walio kusudia na sio kupeleka mahali ambapo hapatakiwi.
“Halmashauri ya mji Njombe inatambua umhimu wa kuwasaidia wanafunzi wa kike ndiomana Baraza la Waheshimiwa Madiwani waliamua kutenga kiasi cha fedha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike wasipate changamoto wakiwa kwenye masomo yao ,niombe walimu mkazifikishe kwa walengwa walio kusudiwa na sio vinginevyo “alisema Mhe Erasto Mpete Mwenye kiti wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Akiendelea kuzungumza Mhe.Mpete amewaasa wanafunzi wote wa Halmashauri ya mji Njombe kuzingatia nidhamu kwa walimu, wazazi na walezi akikemea wanafunzi kujihusha na mahusiano katika umri mdogo jambo ambalo limekuwa likichangia kuharibu maadili.
Aidha katika hafla hiyo kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya mji Njombe ndugu Thadei Luoga amesema taulo hizo zitaenda kuimarisha usafi kwa Watoto,usawa kwa watoto wa kike kupata elimu pia kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike pamoja na kumsaidia mtoto wa kike kwenda kujiamini awapo katika siku zake.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe