Halmashauri ya Mji Njombe Mei 03,2024 imekabidhi mipira 160 kwa ajili ya mchezo wa soka kwa shule za Msingi 16 iliyotolewa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kwa lengo la kukuza na kuendeleza mchezo soka shuleni.
Mkuu wa Idara ya elimu ya msingi na awali Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Shida Kiaramba ameshukuru kupokea vifaa hivyo ambavyo vitakuwa na mchango mkubwa kwenye kuendeleza vipaji vya mchezo wa soka kwa wanafunzi.
"Tunashukuru sana, na sote tunafahamu michezo ni muhimu sana na ili tuweze kupata wachezaji wazuri ni lazima waanzie chini kuanzia shule za Msingi" Alisema
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mipira hiyo kwa maofisa elimu wa kata, Mwenyekiti wa chama cha mpira miguu Wilaya ya Njombe Ndugu Hans Luwanja alisisitiza vifaa hivyo kutumika.
"Tuwaombe mipira hii ikatumike kuendeleza michezo kwenye shule zetu na mipira hii ichakae kwa kutumika badala yakuwekwa makabatini na inapochakaa utafutwe utaratibu wakupatikana mingine." Alisema
Kwa upande wake Ofisa Utamaduni na Michezo Halmashauri ya Mji Njombe Clemence Manga alisitiiza mgawanyo kwenye kata uwe sawa kama ilivyopangwa.
" Tunagawana mipira hii kulingana na ukubwa wa kata na idadi ya shule, tuhakikishe zile shule maalumu zilizochaguliwa kupewa mpira zinapata kusiwepo malalamiko"
Kata ya Mji Mwema, Njombe Mjini na kata ya Ramadhani zimepatiwa mipira 20 kila kata huku kata 10 zilizosali zikipatiwa mipira 10 kila kata.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe