Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kanda ya nyanda za juu kusini imesema inaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinahusu mbolea kwa wakulima.
Meneja wa kanda Ndugu Michael Sanga amesema hayo Septemba 13,2023 wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa kujadili maendeleo kwenye maandalizi ya uuzaji wa mbolea za ruzuku kwa msimu ujao wa kilimo 2023/2024 wilayani Njombe .
Asifiwe Magima mweyekiti wa waauzaji wa mbolea wilaya ya njombe aliwasilisha baadhi ya changamoto kwenye ununuzi na uuzaji wa mbolea za ruzuku ikiwemo changamoto kwa mawakala kucheleweshewa na wengine kutolipwa kabisa fedha walizoweka dhamana kwa baadhi ya makampuni yanayosambaza mbolea Wilayani Njombe.
Akitolea ufafanuzi jambo hilo meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA kanda ya nyanda za juu kusini Michael Sanga alisema changamoto hiyo imewafikia na inaendelea kufanyiwa kazi ili wadau hao waweze kupatiwa haki yao.
“Kuhusu bond ni kweli wapo ambao hawajalipwa na zipo changamoto ambazo zilijitokeza kwa baadhi ya wauzaji kushindwa ku SCAN QR CODE hili ni tatizo maana mzalishaji hawezi kulipwa bila mauzo yake kuonekana ,tunaendelea kushughulikia maana wapo ambao tayari wamelipwa fedha na wengine mbolea kuendana na thamani ya fedha na hapa itafanyika.”
Wakati akihitimisha kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa alitoa siku saba kwa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea Tanzania TFRA kuhakikisha inatoa majibu ya lini mawakala wanaodai fedha kutoka kwa makampuni hao watalipwa fedha zao ili wasikwame kuwahudumia wakulima
Katika hatua nyingine Sanga amesema mamlaka ipo kwenye mpango wa kuboresha mfumo wa usajili wa wakulima ili uweze kukubali matumizi ya aina nyingine ya kitambulisho ikiwemo cha mpiga kura ili kupunguza chanagamoto ya sasa kwa wakulima kushindwa kusajiliwa kwenye mfumo kutokana na mfumo kuhitaji mkulima kuwa na kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia NIDA.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe