Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick Ameiaga Timu ya Kurugenzi ambayo inaiwakilisha
Halmashauri ya Mji Njombe kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano ya mpira wa nyavu (volleyball)
Akizungumza na timu hiyo Agosti 28,2024 akiwa ofisini kwake Mkurugenzi ameiomba timu hiyo kwenda kuipeperusha vyema bendera ya Halmashauri ya Mji Njombe kwa kuibuka kidedea katika mashidano watakayo shiriki.
Kwa upande wake Robert Sanga Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo amesema wamejipanga vilivyo kwenda kukabiliana na wapinzani watakao kwenda kukutana nao katika mashindano hayo na kuahidi kufanya vyema kutokana na ubora wa kikosi walicho nacho cha mashindano.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe