Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Oktoba 18,2023 imefanya mafunzo kwa kamati ya uchunguzi wa madhara makubwa yanayodhaniwa kusababishwa na dawa na vifaa tiba kwa wataalamu wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Mji Njombe.
Mafunzo hayo yametolewa na mkaguzi wa dawa kutoka TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bi. Grace Kapande kwa wafamasia ,madaktari ,wataalamu wa maabara,waratibu wa chanjo na wauguzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Mji Njombe.
Bi.Grace ameeleza kuwa timu ya Mkoa inajukumu kubwa la kuhakikisha taarifa zote za madhara yatokanayo na dawa na chanjo zinafanyiwa uchunguzi nakutolewa taarifa kwa mamlaka ili hatua ziweze kuchukuliwa
“Hii timu mna jukumu kubwa la kuhakikisha mnafahamu pindi madhara yapojitokeza na kutolea taarifa kupitia fomu maalamu au kwa njia ya simu pia ni jukumu lenu kuhakikisha mnafanya uchunguzi na kuratibu shughuli zote zinazohusu dawa,chanjo na vifaa tiba kwenye mkoa”Alisema Bi Grace Kapande.
Aidha amesema madhara yanayotakiwa kufanyiwa uchunguzi ni madhara makubwa ambayo yangeweza kusababisha kifo,ulemavu wa kudumu pamoja na madhara ya aina moja yanayotokea kwa wingi.
Katika hatua nyingine wataalamu hao wametakiwa kuendelea kushirikiana na wananchi kwa kuwapatia elimu ili waweze kutambua umuhimu wa kutoa taarifa za madhara yatokanayo na dawa na chanjo.
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya Afya yenye jukumu la kusimamia ubora ,usalama na ufanisi wa dawa ,vifaatiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe