Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Njombe Bw. Lewis Mnyambwa kwa niaba ya katibu Tawala Mkoa wa Njombe Februari 23,2024 amefungua mafunzo ya siku moja kwa wafamasia, wamiliki na wasimamizi wa Famasi na maduka ya dawa za binadamu pamoja na dawa za mifugo kutoka Mkoa wa Njombe.
Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja ili kuboresha mifumo ya ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba ili kuwa na dawa pamoja na vifaa tiba bora kwa wananchi.
Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya nyanda za juu kusini wakiongozwa na Bi. Anitha Mshighati ambaye ni Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe