Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mheshimiwa Filoteus Mligo aimetaka jamii kutunza mazingira pamoja na kufanya usafi kwenye maeneo yao ya makazi ili kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Amesema hayo Mhe.Mligo Januari 30,2024 wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani kujadili taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Ameeleza kuwa kipindi hiki cha mvua ni kipindi ambacho kinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kuhara na kipindupindu hivyo jamii ichukue tahadahri kwa kuhakikisha mazingira yanatunza na kuwa safi wakati wote.
Aidha amewataka wafanyabiashara wote wa vyakula ,mamalishe na babalishe kuzingatia usafi kwenye maeneo yao ya biashara ili wasiwe chanzo cha mlipuko wa magonjwa huku akiielekeza idara ya afya Halmashauri ya Mji Njombe kushirikiana na kitengo cha usafi wa mazingira kuwawajibisha wale wote ambao watakiuka sheria na kanunui za usafi wa mazingira kwenye maeneo yao ya biashara.
Katika hatua nyingine amewataka wataalamu kushirikiana na waheshimiwa madiwani kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza pato la Halmasahuri.Aidha amesisitiza wataalamu kuhakikisha miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye kata zote inakamilika kwa wakati na thamani ya mradi inaonekana ili kuwezesha Halmashauri kupata fedha zaidi kutoka Serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo.
Mhe. Mligo pia amewataka madiwani kuhakikisha wanafuatilia miradi hiyo kwa ukaribu sambamba na kuzifuatilia kwa ukaribu kamati za ujenzi ambazo zinasimamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Sambamba na hayo Makamu Mwenyekiti Mhe.Mligo amewataka wananchi wote Mjini Njombe kutumia vizuri mvua ambazo zinaendelea kunyesha kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo miti ya matunda ,biashara ,mampamobo pamoja na miti mingine rafiki wa mazingira ili kuendelea kupendezesha na kutunza mazingira ya Mji wa Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe