Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Ndugu Agatha Mhaiki amewataka wananchi wa kijiji cha Igoma kilichopo kata ya Iwungilo Halmashauri ya Mji Njombe kuachana na Imani za kishirikina na badala yake waendelee kudumisha amani na upendo ambayo ni tunu ya taifa letu.
Ameyasema hayo Januari 17 ,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara, uliolenga kuondoa sintofahamu iliyojitokeza kwa baadhi ya wananchi na kanisa Lighthouse Mission Church (LMC)
lililopo eneo hilo, kuwa linachangia kuharibu maisha ya baadhii ya wananchi katika eneo hilo.
Akitatua mgogoro huo Bi. Agatha amesema, Serikali haitafunga kanisa hilo na kila mtu anahaki ya kuabudu sehemu ambayo yeye anahitaji bila ya kuvunja sheria za nchi au kwenda kinyume na tamaduni za mitanzania.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe