Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete ametoa rai kwa wananchi wa kata ya Njombe Mjini kushirikiana na Serikali kwenye maendeleo.
Akizungumza Januari 04,2024 na wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika, kusikiliza na kutoa majibu ya kero za wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani, Mhe. Mpete amesema , Halmashauri ipo kwenye mpango wa kufufua Soko la Dodoma kwa kuhakikisha kunakuwa na usafiri wa uhakika kufikia soko hilo.
Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mali mbichi mitaani kujiandaa na kutoa ushirikiano kuhamia Soko la Joshoni kwakuwa soko hilo linafikika baada yakukamilika kwa barabara kuzunguka soko hilo.
Aidha amewasihi wananchi wa Njombe Mjini kuendelea kuwaombea viongozi ambao wanapambana usiku na mchana kuhakikisha maendeleo yanawafikia.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe