Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick amewataka Wajasiriamali walioshiriki kwenye Maonesho ya Utalii karibu kusini kutoka Halmashauri ya Mji Njombe kujifunza na kuongeza maarifa juu ya mbinu mpya, bora na za kisasa kwenye utengenezaji na ufungashaji wa bidhaa mbalimbali ili kuongeza mvuto na upekee wa bidhaa zao.
Kuruthum amesema hayo mara baada ya kutembelea katika mabanda mbalimbali na kujionea shughuli zinazofanywa kwenye maeneo mengine.Aliendelea kusema kuwa licha ya kuwa maonesho ya Utalii yamelenga kutangaza shughuli za Utalii zilizopo katika Halmashauri ya Mji Njombe ni vyema pia kutumia fursa hiyo kujifunza kwa wengine ili kuja na maarifa mapya.
"Hatuwezi kuwa tunafanya mambo Yale Yale kila siku.Ni vyema kutembelea na kuona wengine wanafanya nini ili kuweza kuleta ushindani kwenye soko.Kila siku mambo yanabadilika hivyo maonesho haya yalete tija katika kuboresha bidhaa zetu."Alisema
katika hatua nyingine Kuruthum amewataka Wananchi na Wadau mbalimbali kushiriki na kutembelea katika Banda la Halmashauri ya Mji Njombe ili kujifunza kujifunza vivutio vya Utalii vilivyopo kama vile maporomoko ya mto Ruhuji na Hagafilo,Makaburi ya mashujaa,mioto ya asili,Katika kutangaza vivutio hivyo Halmashauri pia imeambatana na Wajasiriamali Mali waliofanikiwa kupokea Mikopo ya asilimia kumi na kuleta bidhaa ambazo zinaongeza mnyororo wa thamani katika Sekta ya utalii.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe