Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Gwakisa Kasongwa Agosti 12 ,2024 katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe katika Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, ametoa pongezi kwa matokeo mazuri kutoka kwenye alama nyekundu katika kadi alama za utekelezaji wa shughuli za lishe jambo ambalo linaashiria mafaniko kwenye kampeni ya kuhamasisha lishe bora ili kutokomeza udumavu Mkoani Njombe.
" Nitoe pongezi ,kwenye hizi kadi alama inaonesha kazi inafanyika tilipoanza hivi vikao hizi kadi alama ilikuwa nyekundu kila mahali sasa hivi tumepiga hatua kubwa sana ,hongereni wakuregenzi, waganga wakuu maafisa lishe na watendaji tunaenda vizuri."Alisema.MheKissa Gwakisa Kasongwa, Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
Kutokana na changamoto ya hali duni ya Lishe inayopelekea udumavu kwa watoto ,Mkoa wa Njombe unaendelea na Kampeni ya kupambana udumavu ya Lishe ya Mwanao ,Mafanikio yake ,yenye kaulimbiu isemayo "Kujaza tumbo siyo Lishe jali unachomlisha", iliyozinduliwa Disemba 22,2023 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe .Anthony Mtaka ambapo Halmashauri ya Mji Njombe imepiga hatua na hali ya udumavu imepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2022 hadi asilimia 42.4 mwaka 2024 hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo UNICEF na TFNC.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe