• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

TUMIENI TEKNOLOJIA ILI KILIMO KIENDANE NA KASI YA UONGEZAJI THAMANI

Tarehe iliyowekwa: October 24th, 2023

Wakulima mkoani Njombe wametakiwa kutumia vizuri fursa ya maonesho ya SIDO kitaifa yanayoendelea ili kupata teknolojia itakayowawesha kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani mazao yao kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.


Rai hiyo imetolewa Oktoba 23,2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe,wakati wa akifungua maonesho ya nne ya viwanda vidogo SIDO yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba mjini Njombe.


Mhe. Kigahe amesema serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi hivyo ili kuunga mkono jitihada za serikali ni lazima teknolojia iendane sambamba na matarajio ya uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kupata soko la uhakika.


Amesema kuwa muunganiko wa kilimo na viwanda utakuza soko la ndani na nje ya nchi huku akitoa msisitizo kwa Wakulima kuanzisha viwanda Vidogo.


"Kilimo kiendane na kasi ya uongezaji wa thamani ili kudhibiti upotevu wa mazao, tuunganishe kilimo na viwanda itasaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa nje na kuweza kuuza bidhaa zetu nje ya nchi badala yakuuza  malighafi" Alisema Mhe. Kigahe.


Aidha amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO kushirikiana na Halmashauri na kuhakikisha vijana wanapata teknolojia ili kuweza kifanya kilimo kibiashara.


Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wakulima na wajasarimali mkoani Njombe kutumia fursa yakuzungukwa na nchi mbalimbali kutafuta masoko.


"Njombe ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula, tumie nchi jirani zinazowazunguka kama fursa yakujipatia masoko,serikalini itaendelea kufungua mipaka ili kuongeza masoko sambamba na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji pamoja na pato la taifa na mtu mmoja mmoja".


Maonesho ya nne ya Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo SIDO  yalianza Oktoba 21 na yamefunguliwa rasmi Oktoba 23,2023 na Mheshimiwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe na yanatarajia kuhitimishwa Oktoba 31,2023.


Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema  "Pamoja tujenge Viwanda kwa uchumi na ajira endelevu" yanashirikisha wajasarimali zaidi 800 kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. June 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI NJOMBE TC AAGANA NA TIMU ITAKAYOCHEZA SHIMISEMITA.

    August 12, 2025
  • LISHE NA AKIBA YA MAZAO YAHIMIZWA NANENANE.

    August 08, 2025
  • KHERI YA SIKUKUU YA WAKULIMA 88 2025.

    August 08, 2025
  • ELIMU YA UNYONYESHAJI YATOLEWA KWA WAKAZI WA LWANGU

    August 05, 2025
  • Angalia zote

Video

ZIFAHAMU FAIDA ZA HERENI YA KIELEKTRONIKI KWA NG'OMBE.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe