Naibu wa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe.Jumanne Sagini amewataka wataalamu wote watakaotekeleza zoezi la Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaing) kuhakikisha wanafanikisha matarijo ya kampeni hiyo ya kushughulikia kero na changamoto za wananchi.
Mhe.Sagini ametoa rai hiyo Mei 25,2024 wakati akifungua kikao kazi cha mafunzo kwa wataalamu watakaofanya kazi kwenye utekelezaji wa kampeni hiyo kuanzia Mei 27 hadi Juni 04 ,2024 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe .
“ Ninamshukuru sana Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia jambo hili lifanyike,Mama Samia Legal Aid Campaing ni kampeni ambayo ina baraka zote za Mhe.Rais,suala la msaada wa kisheria ni jambo ambalo limeonekana kuwa na umuhimu mkubwa sana kwa wananchi,ninaamini ninyi mlioaminiwa kufanya kazi hii mtathamini uzito huo ambao Mhe.Raisi ameuweka kwenye jambo hili”. Alisema Mhe.Sagini.
Aidha Mhe.Sagini amewasisitiza watalamu hao kufanya kazi ambayo itajibu hoja za wananchi na matarajio ya Serikali.
“Tafsiri ya wananchi kutoa kero kwa viongozi ni kwamba kuna mambo mengi kwenye utekelejazi wa shughuli za umma hayafanyiwi kazi ipasavyo,anapotokea mtu kusikiliza shida yao lazima wajitokeze, kazi mnayoenda kuifanya ni matajiro yetu ikifanyika vizuri watu wakaelewa wakitingwa na jambo gani wanakwenda wapi na wanapokwenda watu wakawa tayari na wakasilizwa vizuri ,hizi tunazoziita kero zitapungua kwa kiasi kikubwa”.
Katika hatua nyingine ametoa rai kwa Wizara ya Katiba na Sheria kupita kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg.Khatibu Kazungu kufanya utafiti mdogo juu ya madhara ya watu kutokufahamu haki zao za msingi kisheria ili uwe ni chachu yakutatua kero ambazo kwa namna moja ua nyingine zinatengenezwa na watumishi wa umma wasiotimiza wajibu wao vizuri.
Njombe ni Mkoa wa 7 kupokea wataalamu wakutoa msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaing).
Kauli mbiu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaing inasema “Msaa wa kisheria kwa Haki, Usawa,Amani na Maendeleo”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe