Watahiniwa wanaojianda na Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba wametakiwa kutumia vyakula rafiki ili wawe na utulivu wakati wakufanya mitihani .
Ameyasema hayo Mhe Erasto Mpete Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Septemba 11, 2023 alipotembelea Shule ya Msingi Mikongo iliyopo Kata ya Kifanya kwa niaba ya shule zote za Halmashauri ya Mji Njombe
Akiwa shuleni hapo alipata fursa ya kuzungumuza na watahiniwa wa Darasa la Saba nakuwaomba watahiniwa hao kuhakikisha wanapata muda wanatumia vyakula ambavyo havitawaletea usumbufu watakapokuwa katika vyumba vya kufanyia mtihani.
Katika hatua Nyingine Mhe.Mpete amewaomba watahiniwa hao kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kupumzika .
“Ninaamini mmesoma na vile walivyowafundisha waalimu wenu vimetosha sasa hivi pumzikeni ili msi paniki”.
Kwa upande wake mkuu wa Idara ya Elimu Halmashauri ya Mji Njombe Shida Kiaramba amesema maandalizi yamefanyika vizuri na wanafunzi wapo tayari kufanya mitihani yao.
“Maandalizi yamekamilika kila kitu kipo sawa shule zetu 95 zimewaandaa wanafunzi kufanya mitihani ,jumla ya wanafunzi watakaofanya mtihani wakuhitimu darasa la saba ni 4,871,wasichana wakiwa 2,522 na wavulana 2,349.”
Wanafunzi wa darasa la saba nchini kote wanatarajia kuanza kufanya mtihani wa taifa wakuhitimu Elimu ya Msingi Mwaka 2023 kuanzia siku ya Jumatano Septemba 13, 2023 na wanatarajia kumaliza siku ya Alhamisi Septemba 14,2023.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe