Ni ujumbe muhimu uliotolewa kwa madereva ,watunza kumbukumbu na wahudumu mbalimbali kwenye ofisi ya halmashauri ya Mji Njombe pamoja na waelimisha rika kutoka kiwanda cha chai cha Uniliver ,wakati wakipatiwa mafunzo ya mpango wa Ukimwi ,magonjwa sugu na magonjwa yasiyo ambukiza mahala pa kazi
Akiwasilisha mada ya afya ya akili kwa washiriki wa mafunzo hayo ,Bi.Joyce Lameck mratibu wa magonjwa ya afya ya akili kutoka hospitali Kibena ametoa rai kwa watumishi hao kujitunza na kuchukua tahadhari ili kulinda afya yao ya akili.
Bi Joyce ,amelitaka kundi hilo kujiepusha na tabia hatarishi ikiwemo ulevi na matumizi ya dawa za kulevya kwani ni mojawapo ya vichocheo vinavyosabisha mtu kupata msongo wa mawazo nakupelekea kupata ugonjwa wa akili.
Aidha amevitaja vichocheo vingine vinavyoweza kusababisha mtu kupata tatizo la afya ya akili kuwa ni pamoja na mtu kufiwa na mtu wake wa karibu,Umasikini ,Migogoro ya kifamilia(ndoa),Upweke,kufukuzwa kazi ,kufeli mitihani au maisha ,kutozaa ,imani za kishirikina pamoja na kutengwa na jamii.
Kwa upande wake mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Daktari Isaya Mvinge ametoa wito kwa watumishi wao kupata muda wa kuchunguza afya zao haswa kwa magonjwa yasiyo ambukiza kwani mengi hayana tiba.
Bi Uria Mtweve, mratibu wa kudhibiti Ukimwi idara ya Afya, Halmashauri ya Mji Njombe ametumia fursa hiyo kukumbusha kundi la madereva juu ya kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi ambapo mkoa wa njombe ni miongoni mwa mikoa yenye takwimu za juu kwenye maambukizi kwa asilimia 11.4
Aidha Bi Uria amesisitiza umuhimu wakupima afya ili kuanza kutumia dawa mapema endapo mtu atabainika kuwa na maambukizi na kujikinga kwa wale watakaooneka kutokuwa na maambukizi.
Baadhi madereva wa halmashauri ya Mji Njombe Hassan Milanzi na Mohamed Mdoe wamesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa wa namna yakujikinga na magonjwa ya akili,VVU pamoja na magonjwa yasiyo ambukiza wawapo kazini na nje ya maeneo ya kazi.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuboresha utendaji kazi na kujenga uelewa wa kujikinga na madhara yatokanayo na afya ya akili,Ukimwi na magonjwa yasiyo ambukiza kazini yametolewa Novemba 04,2023 kwa washiriki 68.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe