Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka amesema mkoa utaendelea kusimamia vyema fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Njombe.
Amesema hayo Oktoba 28,2023 wakati akitoa salamu za Mkoa kwa Mheshimiwa makamu wa Rais Dkt Philip Isdor Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Kilele cha maonesho ya nne ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO yanafanyika kitaifa Mkoani Njombe.
"Miradi yote itaendelea kusimamiwa vizuri fedha yote ya serikali itasimawa vizuri n kuhakikisha thamani ya fedha kwenye mradi unaonekana".
Mkuu wa Mkoa Mtaka ametumia fursa hiyo kuwaonya Wauzaji wa mbolea za ruzuku kuepuka udanganyifu.
"Tutasimamia vizuri mbolea ya ruzuku timu ya mkoa imejipanga wachakachuji tutawashughulikia vizuri." Alisema Mhe. Mtaka.
Kuhusu lishe Mheshimiwa Mtaka amesema kuwa, mkoa tayari umenza kuchukua hatua za makusudi kuhamasisha lishe bora kutokomeza utapiamlo na udumavu, kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Njombe na katibu tawala mkoa wa Njombe.
"Jambo la lishe tumelichukua kwa uzito na tayari DC ameanza na tunaenda kuzindua kampeni hiyo rasmi."
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe