Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick leo amekabidhi fimbo nyeupe ya kutembelea kwa Kijana Sebastiani Kilasi ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa mwenye matatizo ya ulemavu wa macho.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fimbo hiyo maalumu,Sebastian Kilasi mwenye ulemavu wa macho amesema kuwa changamoto aliyokuwa nayo awali ambayo ilimpasa mara nyingi kuongozana na mtu kwa msaada kwa sasa itakwenda kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa fimbo hiyo maalumu kwa walemavu wa Macho.
"Nashukuru sana kwa msaada huu na hata niwapo chuoni ntakua katika mazingira mazuri ya kutokuwa tegemezi, ninapotaka kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwenye vivuko na pia kuwa na pia kujipangia muda wangu vizuri wa kujisomea badala ya kusubiria ratiba za wenzangu."Alisema Kilasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick ametoa rai kwa jamii kuendelea kusaidia wale wote wenye mahitaji mbalimbali kwenye jamii kwa kuwajali ili nao waweze kujiona sehemu ya jamii.
Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe Petro Mahanza amesema kuwa Mpaka sasa Halmashauri imenunua vifaa mbalimbali zikiwemo fimbo nyeupe kumi,baiskeli za walemavu,magongo ya kutembelea walemavu,mafuta kwa wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambavyo vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya shilingi milioni tatu ikiwa ni sehemu ya mapato ya ndani ya Halmashauri
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe