Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji Njombe Dkt. Jabir Juma amewataka watoa huduma ndani ya maduka ya dawa za binadamu kuhakikisha wanazingatia misingi na taratibu ambazo zimewekwa na Serikali za kutoa huduma kwa wananchi.
Yamesemwa hayo na Dkt. Jabir Juma Msonde Februari 7,2024 wakati akifunga mafunzo kwa watoa huduma ndani ya duka la dawa kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Njombe ambapo mafunzo hayo yalilenga kuwakumbusha watoa huduma za dawa kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni ,miongozo na taratibu za uendeshaji wa maduka ya dawa ,kushirikisha matokeo ya kaguzi mbalimbali zilizofanyika na wakaguzi ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na kupeana elimu juu ya vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa ,vifaa tiba na chanjo.
Akiendekea kungumza Dkt. Jabir Juma ametoa onyo kali kwa wale ambao wanauza dawa za Serikali kwenye maduka binafsi sheria kali zitachukuliwa dhidi yao kwani ni uhujumu Uchumi wa nchi na kukiuka taratibu.
Aidha Mganga Mkuu amewaasa watoa huduma za dawa hao kutumia taaluma zao katika kutoa elimu na sio kuwaweka watu ambao hawana taaluma kwenye maduka yao, mwisho kupelekea madhara juu ya wanaoenda kununua dawa kwa mtu ambaye hafahamu ni dawa ipi anapaswa kupewa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe