Diwani wa viti maalumu kata ya njombe Angel Mwangeni amewataka wanawake mkoani njombe kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuzingatia elimu ya lishe ambayo inatolewa na watalamu ili kuunga mkono juhudi za kutokomeza udumavu mkoani Njombe.
Mheshimiwa Mwangeni alesema hayo Novemba 25 ,2023 katika mitaa mitatu ya kata ya Njombe Mjini ambayo ni Kihesa ,Mgendela na National Hausing ambapo amewaomba wananchi kuzingatia lishe na milo yote mitano ambayo inashuruwa kitalaamu.
"kila mwanamke naomba ashike nafasi yake,wanaume wanatutegemea sisi wanawake ,twendeni tukaifuate elimu ya lishe ambayo inatolewa na wataalamu ,na sisi wanawake tupungunze muda mwingi katika kazi zetu na tukasahau malezi ya mtoto "Angel Mwangeni Diwani wa Viti Maalumu Njombe Mjini .
kwa upande wake Bwana Enos Lupimo Mtendaji Kata ya Njombe amesema Serikali imejipanga kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kutokomeza udumavu ambapo kwa Halmashauri ya Mji Njombe imeweka utaratibu wa kuhakikisha kila mwananchi anapanda mbogamboga katika eneo lake la makazi ,kufuga kuku kwa ajili ya kupata nyama na mayai kwa mtoto pamoja na kupanda miti miwili ya tunda la parachichi katika eneo lake
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe