Waandikishaji wa orodha ya wapiga kura wa Serikali za Mitaa 2024 kwenye vituo mbalimbali vilivyopo katika kata za Halmashauri ya Mji Njombe wameapishwa rasmi Tarehe 07 Oktoba 2023 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Njombe.
Kiapo kwa waandikishaji hao kimeongozwa na Hakimu mkazi Isack Mlowe na kushuhudiwa na mashahidi mbalimbali wakiwemo wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata na mitaa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Njombe.
Waandikishaji wameapishwa ili kuhakikisha wana tekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba, Sheria na kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Zoezi la kuandikisha wapiga kura litaanza Tarehe 11- 20 Oktoba 2024 na vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2 Asubuhi nakufungwa saa 12 Jioni.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi ".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe