Mganga Mkuu wa Halmashuari ya Mji Njombe Dkt Jabil Juma amewaombwa wadau na wananchi wote kuendelea kuelimishana umuhimu wa kula mlo kamili wenye makundi yote sita ya vyakula ili kuondokana na tatizo la udumavu katika Mkoa wa Njombe.
Amezungumza hayo Tarehe 07 Juni,2024 katika kikao cha kutathimini utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa Lishe katika Halmashauri ya Mji Njombe kwa Kipindi cha robo ya tatu ya mwaka kuanzia Januari hadi Machi 2024,kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini pamoja na idara mtambuka ndani ya Halmashauri.
“Niwambe sana wadau mliofika hapa ichukueni changamoto ya lishe kama ajenda muhimu katika maeneo yenu mnayoishi,tusaidiane kuibadilisha jamii juu ya mtazamo hasi kuhusu udumavu,wapo baadhi ya watu mpaka sasa hawa amini kama njombe tuna changamoto ya udumavu”.Alisema Mganga Mkuu ,Dkt.Jabil Juma .
Aidha amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata milo isiyo pungua mitatu kwa siku ambayo ina makundi sita ya vyakula.
Kwa upande wake Michael Swai Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Njombe amesema mapambano ya kutokomeza udumavu yanaendelea na Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa kupunguza udumavu kwa asilimia 3 kutoka 45% Disemba 2022 hadi 42% mwaka 2024.
Aidha amesema kitengo cha Lishe kwa kushirikiana na wadau wataendelea kutoa elimu juu ya ulaji unaofaa na kupima hali ya lishe kwa watoto pamoja na kuwajengea uwezo wahudumua katika vituo vya kutolea huduma za Afya, namna ya kupima urefu na kutafsiri ili kuwa na takwimu sahihi katika jamii na vituo vya kutolea huduma za afya.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe