Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka awapongeza walimu wote wa Shule za msingi kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2024 Mkoa njombe umekuwa wa tatu kitaifa.
Pongezi hizo amezitoa Februari 12 2025 wakati Akizungunza na walimu wa Shule za Msingi , Sekondari, Maafisa Elimu na Wadhibiti ubora wote wa mkoa wa Njombe katika hafla ya utoaji wa vitabu vya ziada kwa shule za msingi na sekondari, ambapo Mhe Mtaka aliwapongeza kwa kufanya vizuri katika matokeo ya Darasa la saba kwa mwaka 2024 ambapo mkoa Njombe umeshika nafasi ya tatu kitaifa .
"Niwapongeze walimu wote, mafisa elimu na wadhibiti ubora wote kwa kuwa na mshikamano mpaka tunakuwa vinara kitaifa katika kufanya vizuri kwenye matokeo yote ya Shule za Msingi " Alisema Mhe Anthony Mtaka mkuuu wa Mkoa Njombe
Aidha Mhe. Mtaka amewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa wa njombe kuwapa kipaumbele walimu wanaofika kupata huduma katika ofisinza halmashauri na Hospitali kupatiwa kipaumbele kutokana na uwingi wa wanafunzi ambao amewaacha katika shule ambao anafundisha.
Kwa upande wa mitihani ya darasa la Saba 2024 Mkoa njombe umefanya vizuri katika katika masomo mbalimbali kitaifa ambayo ni somo Kiswahili nafasi ya kwanza Kitaifa ,Maarifa ya Jamii mkoa wa umeshika nafasi 2 kitaifa ,Kingereza Mkoa umeshika nafasi ya 2 kitaifa ,Uraia na Maadili mkoa umeshika nafasi ya 2 kitaifa, Sayansi na Teknolojia Mkoa wa umeshika nafasi ya 2 kitaifa kwenye somo la Hisabati Mkoa umeshika nafasi ya 2 kitaifa .
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe