Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Erasto Mpete ametembelea katika mitaa mbalimbali Mjini Njombe na kujionea shughuli za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zinazofanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA na kuwataka kuharakisha ujenzi huo kabla ya kipindi cha mvua kuanza.
Mpete amepongeza TARURA kwa upande wa Halmashauri ya Mji Njombe na kusema kuwa kwa sasa wanafanya ujenzi wa miradi ya barabara kwa kiwango cha lami katika Mitaa mbalimbali jambo ambalo litasaidia kupunguza changamoto ya ubovu wa barabara na pia kupunguza vumbi lililokuwa likiwatesa Wananchi ambao makazi au biashara zao zipo pembezoni mwa barabara ambao walikuwa wakipata kero kubwa.
Aidha katika hatua nyingine Mpete amewasihi Wananchi kuhakikisha kuwa wanatunza mitaro na kusafisha mitaro ambayo inajengwa pembezoni mwa barabara hizo badala ya kutumia mitaro hiyo kutupa taka na kuhifadhi taka jambo ambalo linasababisha kuziba na kushindwa kupitisha maji kipindi cha mvua na kupelekea maji kupoteza mweleko na kuingia kwenye makazi ya watu.
Kwa upande wake Meneja TARURA Wilaya ya Njombe Safari Alex amesema kuwa kwa upande wao watahakikisha wanaendelea kufanya usimamizi wa karibu katika miradi hiyo ya barabara ili ikamilike kwa ubora na kwa wakati.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe