Halmashauri ya Mji Njombe imeanza ujenzi wa vyumba 26 vya madarasa kwa shule za Sekondari katika Kata 10 ikiwa ni utekelezaji wa matumizi ya shilingi milioni 520 fedha kutoka Serikali kuu na utekelezaji wa agizo la Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kuwa ndani ya siku 75 vyumba hivyo vya madarasa vinakamilika.
Akizungumza katika ziara ya kukagua shughuli za ujenzi katika shule 10 zilizopokea fedha hizo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mheshimiwa Kissa Gwakisa amesema kuwa lengo ambalo Wilaya imejiwekea ni kuhakikisha kuwa madarasa hayo yanakamilika kwa wakati na kuwa ubora unaotakiwa.
"Tumekubaliana kama Wilaya kwenye Halmashauri tatu Halmashauri ya Mji Njombe,Makambako na Wilaya ya Njombe kuwa Ijumaa tuwe tumekamilisha ujenzi wa misingi kwenye maeneo yote na pia Jumanne ya wiki ijayo tuanze zoezi la kupandisha kuta.
Kila mtu ahakikishe anajukumu la kusimamia na pia niwaombe Waheshimiwa Madiwani ambao wanamiradi kuwakutanisha Wananchi kwenye eneo lenye mradi na kuwaonesha shughuli kubwa ambayo kama sio fedha tulizopatiwa basi ingekuwa ni jukumu lao kuchangia fedha hizo hivyo nao pia wanapaswa kujitolea nguvu kazi na kuonesha kuguswa kwao na jitihada hizo"Alisema Kissa
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema Nestory Mahenge ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha hizo ambazo katika Kata ya Mjimwema kuna ujenzi wa vyumba vya Madarasa 2 katika Shule ya Sekondari Mpechi.
"Sisi tutahakikisha tunasimamia kikamilifu zoezi hili na pia tukamilishe kabla ya wakati.Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa fedha hizi Shule ya Sekondari Mpechi kila mwaka tunakuwa na ongezeko na Wanafunzi hivyo tunahitaji Madarasa na pia imetupunguzia uchangiaji wa Wananchi"Alisema Mahenge
Halmashauri ya Mji Njombe imepokea kiasi Cha Shilingi milioni 520 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 26 vya Madarasa ambapo ujenzi wa misingi unaendelea katika Shule hizo
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe