Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa viongozi kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii ili kuondoa tatito la udumavu kwa haraka.
Ametoa maelekezo hayo Januari 27,2024 kwa njia ya simu baada yakupokea salamu za kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa kutoka Mkoa wa Njombe kwenye kilele cha kampeni ya kuongeza kasi yakupunguza udumavu Mkoani Njombe, Kampeni ambayo ilizinduliwa Disemba 22,2023 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka.
“Mi nikushukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa wazo hilo na niwashukuru viongozi wote wa chama Mkoa na Serikali kwa wazo hilo la kukutana na kutafakari suala la lishe, niwaombe sana muendeleze elimu kwa umma, umma ukituelewa basi tatizo hilo litaondoka haraka,” Alisema Rais Dk. Samia.
Kampeni ya Lishe ya Mwanao Mafanikio yake ni kampeni endelevu kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe ambapo uzinduzi kwenye wilaya na Halmashauri zote umefashika na hatua zinazofuata ni kutoa elimu ya lishe ngazi ya kata,mitaa na vijiji.
Kauli mbiu ya Kampeni hiyo inasema “Kujaza Tumbo sio Lishe,Jali unachomlisha.”
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe