Hayo yalisemwa wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika Mtaa wa Mgendera Halmashauri ya Mji Njombe ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usafi duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 21 Septemba ambapo Wananchi wa Mtaa huo kwa Kushirikiana na wadau wa mazingira na Wataalamu walishiriki katika kufanya usafi katika eneo ambapo awali lilikuwa linatumika kama eneo la kutupia taka (Dampo).
Akizungumza na Wananchi mara baada ya kukamilika kwa zoezi la Usafi Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji Njombe Nelson Mlwisa alisema kuwa Wananchi wengi wamejitokeza kufanya usafi jambo ambalo linaonyesha wazi ni kwa jinsi gani uchafu umekuwa kero kwa jamii na jamii imekuwa ikielimika na kustaarabika kila siku.
“Watu wengi wamejitokeza kufanya usafi katika eneo hili ambalo awali lilikuwa dampo. Mkakati wetu kama Halmashauri ni kuhakikisha kuwa tunaimarisha usafi katika eneo hili muda wote kwa kuzuia watu kutoendelea kutupa taka. Yupo mdau ambaye amejitokeza kwa ajili ya kuliendeleza eneo hili kwa kupanda bustani za maua” Alisema Nelson.
Joseph Mtegea ambaye ni mdau wa mazingira kutoka shirika la SHIPO amesema kuwa licha ya kushiriki mara kwa mara katika kufanikisha shughuli za usafi lakini kama wadau kupitia kitengo cha SMART wamekuwa wakitoa elimu ya mara kwa mara juu ya utunzaji bora wa mazingira kwa kutumia teknolojia na mbinu bora za Kilimo zisizo na athari kwa Mazingira.
Eda Kindole, Rosemeria Sanga Ni wakazi wa Mtaa wa Mgendera ambao wao wamepongeza zoezi la usafi lililofanyika katika eneo la lilipokuwa dampo la zamani katika Mtaa huo kwani wamesema kuwa eneo hilo lilikuwa hatarishi kutokana na aina ya taka zilizokuwa zinatupwa katika eneo hilo.
Jumla ya Wananchi 206 waliweza kushiriki katika zoezi la usafi huku mifuko 540 sawa na Kilogramu 3141 za takataka zikiwa zimekusanywa na kupelekwa eneo la dampo kuu lililopo Maheve, Huku wadau wa mazingira wakiwemo shirika la Nipe fagio, wakishiriki kwa kutoa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe