Kampeni ya siku 14 za usafi ndani na nje ya soko kuu la Mji wa Njombe iliyoanza Februari 13,2024 imehitimishwa Leo Februari 24,2024 na Viongozi mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Deo Mwanyika, Mheshimiwa Diwani wa kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa, Katibu Tawala wilaya ya Njombe Ndugu Agatha Mhaiki na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Kuruthum Sadick wameshiriki kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya soko kuu Njombe.
Aidha katika siku hii wananchi wamefanya usafi wa pamoja kwenye maeneo yao ya biashara, maeneo ya wazi, makaburini na maeneo ya makazi ikiwa ni utamaduni wa Mji wa Njombe kufanya usafi wa pamoja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe