Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango, amesema serikali imepanga kujenga uwanja mkubwa wa ndege Mkoani Njombe.
Mheshimiwa Mpango ametoa kauli hiyo ya serikali Oktoba 28,2023 wakati akihitimisha maonesho ya nne ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe.
Amesema serikali inatambua fursa mbalimbali zilizopo mkoani Njombe na umuhimu wa usafiri na usafirishaji hivyo serikali imeamua kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa ndege Mkoani Njombe.
Mheshimiwa makamu wa Rais amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege Njombe utahusisha ujenzi njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilometa Tatu (3), Jengo kubwa la abiria na Jengo maalumu kwa ajili yakuhifadhi bidhaa zinazoharibika haraka.
"Sisi serikali tunaamini uwepo wa usafiri wa uhakika utachangia kuinua na kukuza uzalishaji viwandani na mashambani lakini pia kuinua sekta ya utalii mkoani Njombe."Alisema Mheshimiwa Mpango.
Uwanja wa ndege utakao jengwa mkoani Njombe utakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa za abiria pamoja na ndege za mizigo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe