Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe.Zainabu Katimba Septemba 11,2024 ametoa wito kwa watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika miundombinu na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada yakukagua miundombinu ya kituo kipya cha Afya Muungano kilichopo Kata ya Kifanya, Naibu Waziri amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imewekeza zaidi ya Bilioni 2 kwenye sekta ya Afya ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe kwenye miundombinu na vifaa tiba, hivyo ni lazima uwekazaji huo uendane na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
"Tutoe huduma bora zinazoendana na uwekezaji uliofanywa na Serikali yetu chini ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan,uwajibikaji kwa watumishi ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya, kulingana na maendeleo makubwa yaliyofanyika kwenye miundombinu na vifaa tiba"Alisema Mhe.Zainabu Katimba
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Septemba 11,2024 ilikagua miradi miwili ya Afya ambayo ni ujenzi wa Kituo cha Afya Muungano Kifanya na Ujenzi wa Jengo la Mama na mtoto lenye chumba maalumu kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Halmashauri ya Mji Njombe miradi ambayo umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 770.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe