Halmashauri ya Mji Njombe imetoa kiasi cha shilingi laki tano kwa shule ya Sekondari Uwemba na Njombe Sekondari kwa kufanikiwa kufuta sifuri katika matokeo ya kidato cha sita 2022.Akizungumza wakati wa kufanya makabidhiano hayo kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Erasto Mpete ametoa pongezi kwa Waalimu kwa jitihada kubwa walizozionyesha za kuhakikisha kuwa shule hizo zimefuta sifuri katika matokeo ya kidato cha sita jambo ambalo limezidi kuiongezea Halmashauri heshima kwa kuwa na ufaulu wa juu.
Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kupokea motisha hiyo Jimmy Ngumbuke Makamu Mkuu wa Shule Njombe Sekondari na Johnsia Ngailo Makamu Mkuu wa Shule ya Uwemba wamesema kuwa Uwepo wa sifuri katika shule zao ni miongoni mwa mambo ambayo yaliwafanya kukosa usingizi kwa muda mrefu ambapo kwa kuweka mikakati iliyo bora miongoni mwa Waalimu na Wananfunzi kwa kushirikiana walifanikiwa kufuta sifuri kwenye matokeo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa mazoezi ya mara kwa mara,waalimu kuendelea kutoa msaada kwa kusaidia wanafunzi hata baada ya masomo na kuongeza bidii katika ufundishaji na usimamizi wa nidhamu jambo lililopelekea uwepo wa matokea hayo
Naye Diwani wa Kata ya Uwemba Jactan Mtewele amesema kuwa kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Uwemba uwepo wa matokeo hayo umekuwa na faraja kubwa kwa wazazi kwani uwepo wa sifuri ulikuwa unatia doa lakini kwa sasa imani ya wazazi na wanafunzi juu ya ufaulu wa shule hiyo umeanza kurejea na kama Diwani atahakikisha anashirikiana na uongozi wa shule kutatua changamoto shuleni hapo ili shule hiyo iweze kuendelea kusikika vyema kwenye ufaulu Nchini.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe