Kuelekea Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Halmashauri ya Mji Njombe imefanya mdahalo katika chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Njombe kujadili jitihada za Serikali kwenye maendeleo na kumwinua mwanamke na mtoto wa kike kiuchumi.
Akizungumza Marchi 01,2024 Bwana Geophrey Kaduma kutoka ofisi za msaada wa kisheria Wilaya ya Njombe (NJOPACE) katika uzinduzi huo amesema, lengo la kuweka wiki ya maadhimisho ya mwanamke duniani ni kutambua nafasi ya mwanamke kwenye jamii, katika malezi ya watoto pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali kuwinua wanawake kiuchumi.
Kwa Upande wake Ahaz Kinyamagoha afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Njombe maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yataadhimishwa kwa siku saba kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo,kutoa msada kwa wahitaji katika gereza la Wilaya ya Njombe ,kutoa msaada kwa wanafunzi wa mahitaji maalumu katika shule ya msingi kibena pamoja na kufanya usafi katika kituo cha afya mji mwema.
Aidha Sadock Daudi mratibu wa mafunzo chuo cha maendeleo ya wananchi Njombe amesema kama chuo watahakikisha mafunzo ambayo wanayatoa yanampatia mwanamke ujuzi ambao utamsaidia katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali mara baada ya kumaliza mafunzo.
Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yanaambatana na kauli mbiu isemayo “Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii”.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe